Menu
Read More
Read More
Read More

About Jikinge

Jikinge is a program desined to empower individuals to lead healtheir and more fulfilling lives

Through a holistic approach we aim to promote physical and mental wellness ethical decision making and personal growth.The program provides practical resources and expert guidance to empower participants to take control of their wellbeing

  • Many fail to find protection by seeing the verse
  • Others fail to gain immunity due to the distance of access
  • Others fail to get immunity for failure to pay
Explore Now
  • 135
  • Customers
  • 106
  • Services
  • 185
  • Phone Supports
  • 15
  • Customer care

what we do

Jikinge Main Programs

  • Workshops

    We conduct engaging workshops that cover a range of topics, from health to personal development and growth.

    01
  • 02
    Consultancy and Counseling

    Our professional services offers support to individuals, couples,families and groups.

  • Awareness Campaigns

    Through different campaigns we aim to raise consciousness about critical issues affecting our communities

    03
  • 04
    Health Resources

    We provide valuable health resources that equip individuals with tools needed to make informed decision.

Request service

FAQ'S

Frequently Asked Question

Kondomu ni kifuko kilichotengenezwa na mpira laini ambacho hutumiwa wakati wa kufanya ngono. Huvishwa kwenye uume uliosimama hivyo manii yanavyotoka kwenye uume huo wakati mwanaume anapofikia mshindo huzuiwa humo. Kondomu hutumika kama njia ya kuzuia ujauzito na pia hutumika kuzuia maambukizi yakiwemo ya VVU (virusi vinavyosababisha UKIMWI), kwa sababu huzuia uke usipate majimaji yatokayo kwa mwanaume na pia huzuia uume usipate majimaji ya mwanamke. Kondomu zimetengenezwa kwa mpira unaonyambulika kirahisi kutosha karibu kila uume. Pia zipo kondomu za kike huvaliwa kwenye uke kabla ya kufanya ngono.

Unatakiwa kuanza kutumia kondomu kuanzia mara ya kwanza unapofanya ngono, na kila unapofanya ngono endapo unataka kujikinga na mimba zisizotakiwa na maambukizi yatokanayo na ngono kama VVU. Huu ni wakati mzuri kwenda sehemu itoayo huduma za afya kupata ushauri kuhusu njia nyingine za uzazi wa mpango na kujikinga na magonjwa ya ngono. Hata hivyo, uvaaji wa kondomu unahitaji mazoezi ili ujiamini vya kutosha kuhusu kutumia kifaa hicho. Hii ndiyo maana watu wengine hufanya mazoezi ya kuvaa kondomu, hata kama bado hawajaanza ngono.

Unaweza kupata kondomu kutoka kwenye sehemu za huduma za afya, maduka ya dawa na maduka mengine makubwa na madogo. Kondomu za bure zinaweza kupatikana katika sehemu za umma zinazotoa huduma za afya. Kondomu zijulikanazo kama " Salama " zinagharirnu kati ya sh. 100 na 200 kwa tatu na zinaweza kununuliwa kwenye maduka ya dawa, vioski na maduka mengine. Aina nyingine za kondomu zinauzwa hadi kufikia sh. 1000. Hata hivyo hii haimaanishi kuwa hizi ni bora zaidi.

Ili kutumia kondomu, unatakiwa kufuata hatua zifuatazo:
  • Kwanza hakikisha kuwa pakiti ya kondomu iko katika half nzuri na uifungue kwa uangalifu kwenye moJa ya kona zake. Angalia usichane kondomu kwa kutumia vitu vyenye ncha kali.
  • Wakati uume ukiwa umesimama, minya chuchu ya kondomu ili kuweza kutoa hewa iliyopo kwenye kondomu hiyo kabla ya kuikunjua na kuivaa. Hii inazuia kondomu kupasuka.
  • Kisha kunjua kondomu kwenye uume uliosimama ukiacha nafasi kwenye chuchu ya kondomu. Wakati unavaa kondomu hakikisha kuwa ule mkunjo wa kondomu uko nje, ama sivyo haitakunjuka. (Ikitokea kwamba umevaa kondomu nje ndani ivue na uvae nyingine mpya). Endelea kukunjua kondomu mpaka itakapofika kwenye shina la uume. Wanaume ambao hawajatahiriwa wanashauriwa kuvuta nyuma govi kabla ya kuuvalisha kondomu uume wao.
  • Ukishahakikisha kuwa kondomu imevaliwa vyema, unaweza kuanza kufanya mapenzi kwa usalama.
  • Ukishafikia mshindo, shikilia kondomu kwenye shina la uume na ondoa uume kutoka kwenye uke kabla uume haujasinyaa (haujalegea). Vua kondomu kwa uangalifu bila kumwaga manii.
  • Funga fundo kwenye kondomu kisha itupe kwenye choo cha shimo au ichome na usiitupe hovyo. Tumia kondomu moja katika tendo moja la ngono na siyo matendo zaidi!